Breaking

Friday, June 5, 2020

Power Mabula: Mtu Aliyetikisa Enzi zake....Kwa Nguvu Alizonazo za Kuzuia Lorry Kwa Nywele zake

Aisee huyu jamaa alivuma sana miaka ya 80 but sadly I never got to see him. Kulikuwepo na story kibao kuhusu uwezo wake wa nguvu za misuri, mambo kibao yaliongelewa, mfano:

-- Alikuwa anaweza kunywa kreti nzima ya soda kwa mkupuo
-- Alikuwa anaweza kutegesha kifua na tairi la nyuma la trekta kupita bila kuumia
-- Alikuwa anaweza kuvuta lorry lenye shehena kubwa kwa kutumia nywele
-- n.k.

Were these just a bunch of childish myths kutufanya tukimbie mchakamchaka na kuwahi namba shuleni or was there a grain of truth in them? Tafadhali sana naomba wale waliobahatika kuyaona maonesho ya jamaa watupatie ushuhuda hapa.

Pia naomba kuuliza, je yuko wapi siku hizi, kuna mwenye picha? Bado yupo, au..??
Akhsanteni!! By Steve Dii

"Ni kweli huyo jamaa, alikuwa na nguvu kweli kweli, nasikia alikuwa ni mtu wa Musoma, Mara uko...! Hayo ni mambo ambayo kweli alikuwa anafanya, na alikuwa ana uwezo wa kunywa chupa za orange squash mpaka mbili bila ya kuzimua.

Si hivyo tu, alikuwa anauwezo wa kuzuia piki piki kwa kutumia nywele na wakati mwingine meno. Na hata kuzuiya gari kwa kutumia nywele zake. Na alikuwa akivunjiwa jiwe kubwa kifuani kwake.

Pia kulikuwa na mwingine anaitwa power Bernard, na wakaja mwishoni mwishoni kina power Bukuku, ila wengine nimewasahau. By  X-PASTER

"nilimuona mara kadhaa kwenye maonesho wakati nikiwa primary skul. ni kweli alikuwa anafanya hayo yote yaliyotajwa,ilikuwa inaogopesha aisee.mara ya mwisho niliskia habari zake kuwa aliokoka na akatolewa mapepo mengi.

Ilisemekana alikuwa anatumia nguvu za giza na hizo kreti za soda walikuwa wanakunywa majini (sijamuona live baada ya kuokoka).ila naskia aliacha mazingaombwe.umenikumbusha mbali sana
By King'asti

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

1 comment:

  1. Ni kwelli huyu jamaa alikuwa na uwezo huo, mi pia nilibahatika kumuona miaka ya 1970's Shinyanga. Ninachokifiria kwa sasa hivi alikuwa anawezaje kunywa Orange Squash (kinywaji cha enzi hizo) bila kuchanganya maana uchachu wake ulikuwa ni hatari.

    ReplyDelete