Breaking

Friday, September 4, 2020

UTAMU WA MAMA Sehemu ya 62

 

UTAMU WA MAMA SEHEMU YA 62
MTUNZI: GODFREY GODSTAR
CONTACT: 0622177392
FB PAGE: https://www.facebook.com/godstaronline/
AGE:18+
SEHEMU YA 62

ILIPOISHIA.

"mdogo wangu unamuweka katika fungu gani na wewe hapo ulipo sasa unatafutwa,unadhani angel akilijua hili si nitamkosa mdogo wangu kwa umalaya wako huo mwana kunyonyoka wewe"

ENDELEA NAYO.

hakika lilikuwa ni jambo la kusikitisha sana pindi suala ili lifikapo masikioni mwa watu,masumbuko mimi nilijilaumu sana kwa mambo haya machafu niliyoyafanya na ndipo nikaukumbuka ule msemo unaosema dunia tambala bovu ila nikajisemea,dunia sio tambala bovu ila sisi walimwengu ndio wabovu.

madamu alinyanyuka pale alipokuwa na harakaharaka akaelekea ukumbini mahali ambapo yupo angel,na mimi nikawa kama mkia vile nilimfuatilia nyuma nyuma,baada ya kumuona angel yupo chini amezimia ndipo nikakumbuka kile kishindo nilichokisikis muda fulani hivyo ikanilazimu kumuuliza madame imekuwaje.

"nilimpushi wakati saa zile nilipokuwa nakuja kwako nikiwa nimeshika kisu,hivyo sikujua kama amepoteza fahamu"

mmh nilibaki naguna na jitihada za kuirudisha fahamu ya angel iliendelea,tulimpepea sana na kuiamsha mishipa yake ya fahamu kwa kadri ya uwezo wetu na mungu alijaalia tukafanikiwa,angel alipata fahamu ila cha ajabu kitu cha kwanza kukumbuka pindi alipopata fahamu alimuuliza dada yake kuhusu mimi.

"dada masumbuko wangu..mzima"

"huyo hapo nyuma yako"

madame vero alimjibu angel kishingo upande sana.

husiku wa siku hiyo kwangu haukuwa usiku wenye furaha na amani ila ulikuwa ni usiku mrefu sana wenye mawazo mengi kichwani mwangu,ulikuwa ni usiku wenye masikitiko na majuto kwangu,nilikuwa naiwaza kesho yangu,nilikuwa najiuliza kesho yangu itakuwa ni ya uraiani au ya jela.

wakati nikiwa katika dimbwi zito la mawazo mlango wa chumba changu ulifunguliwa na nilipopiga jicho alikuwa ni madame vero na nilipoangalia saa ya ukutani ilikuwa ni saa saba kasoro usiku.

"mbona bado uko macho haujalala"

aliponiuliza hilo swali madame sikumjibu chochote maana nilikuwa naona ananiuliza swali la kipumbavu ambalo majibu yake anayo yeye mwenyewe.

"masumbuko mpenzi wangu,nimekaa nimefikiria nimeona sipaswi kukulaumu sana,wewe ni kijana ambae upo kwenye ujana ambao unachemka,teyari maji nishayavulia nguo sina budi kuyakoga tu"

kwa muda huu nilikuwa niko makini kumsikiliza madame anachotaka kuniambia ni kipi hasa ambacho amekuja nacho usiku huu.

"masu..kijiji au tuseme vijiji ni vidogo sana,suala la angel kwangu halina wasiwasi nitalimaliza mimi mwenyewe ila kipengele ni wazazi wa swaumu na hilo ndio tatizo ambalo linatupaswa kulikwepa kwa haraka"

ndipo na mimi nikajikuta nafunua kinywa changu huku nikiwa nimepata kanguvu kadogo,nikamwambia madame anisaidie kwa hili.

"na ndio lengo la kuja asahivi chumbani kwako,muda ambao swaumu amelala kabisa,alfajiri nitakupeleka stendi tandahimba na pale nitakuacha utachukua gari ya kutoka hapa wilayani tandahimba na uende sehemu yoyote hadi pale janga hili litakapoisha sawa masu"

sikuwa mbishi kwakweli nilimkubalia bila vikwazo vyovyote,alinitazama sana usoni kisha akaniambia.

"mmmh nakuonea huruma sana,mpenzi wangy,pumzika"

chaajabu alinipa busu na kuniambia bado nakupenda sana.

alitoka chumbani na kuniacha nikiwa nimelala.

wanadi swala wa misikiti wa alfajiri walikuwa wanaadhini,hakika nilikuwa nazisikia vyema sauti za waadhini,hivyo niliamka na kwenda kuoga,wakati natoka kuoga na kuingia chumbani kwangu gafra na madame na yeye aliingia hakiwa amevaa kanga yake moja na nguo zingine akiwa amezishika mkononi.

"ooh nilijua bado umelala maana na mimi nimeamka mapema sana nikaoga,hivyo nimekuja huku nataka nivalie nguo huku"

jamani wanawake hawa sijui wakoje,basi madame vero alianza kuvaa ila cha ajabu aliishika chupi yake nyeupe mkononi.

"masu..nimechoka naomba uje kunivalisha hii chupi"

kwakweli kabisa akili yangu wala haikuwa kwenye ngono ila duwa zangu zilikuwa ni kutoka salama katika hichi kijiji na wilaya kwa ujumla.
basi nilienda na kumvalisha chupi yake,alionyesha sura ya tabasamu na mwisho akaniomba msamaha.

tulitembea umbali mfupi kwa mwendo wa gari mpaka kufika wilayani ambako ndio stendi kuu ya magari yanayoenda mtwara mjini,masasi,newala na dar.

tukiwa ndani ya gari kabla ya mimi kushuka madame vero aliniambia maneno machache na yenye busara.

"masu maisha ni hatua,maisha ni safari ndefu sana na kila mmoja mungu humpangia lake la sasa na la baadae pia"

nilishindwa kumuelewa madame hivyo ikanibidi nimuuluze anamaanisha nini.

"namaanisha huvi,angel anakupenda sana tena sana na hata mimi nakupenda ila naamini upendo wa angel ni zaidi na yupo teyari wewe kuwa baba halali wa mtoto atakayezaliwa,unaondoka ila tambua nyuma umemuacha msichana mwenye ujauzito wako"

nilimuitikia kwa kutikisa kichwa.

"sinamaana utoe huduma ila ninachotaka mimi ni mtoto kuwa na baba tu,suala la huduma kwangu ni suala dogo,nitamuhudumia mdogo wangu hadi nahakikisha anajifungua salama kwa uwezo wa mungu,mimi nakupenda sana masu,nimekubaliana na hayo yote sababu wewe ni mwanaume wa pekee sana hasa unapokuwa kitandani"

madame vero aliidaka shingo yangu na kuishikilia ipasavyo aliketa ulimi wake na mimi sikutaka kumuonyesha unyonge nilimpokea na kubadilishana mate kwa sekunde kadhaa.

baada ya hapo alichomoa kiasi kikubwa cha pesa akanipatia pamoja na simu ndogo ya tochi aina ya nokia.

"chukua hizi pesa,ili huko utakapofika ujue pakufikia na ikusaidie kidogokidogo ni shilingi laki 5 na hii simu nimeweka laini yangu nyingine ambayo huwa siitumii mara kwa mara hivyo tutakuwa tunawasiliana na pia ukiwa umekwama kimahitaji nitakuwa nakutumia pesa sawa mume wangu"

nimuitikia na kumshukuru sana hadi nikajikuta natokwa na machozi kwakweli juu ya wema wa huyu dada,hakika nilisema sitomsahau kabisa.

alinifuta machozi na kunikumbatia,niliteremka kwenye gar yake na mimi nikaingia kwenye gari ya kuelekea mtwara mjini na kumshuhudia madame akiondoka.

wakati nimeketi kwenye siti ya gari ambayo inaelekea mtwara mjini gafra kuna wazo lilinijia na nikateremka haraka na kupanda kwenye gari nyingine ambayo inaitwa Buti la zungu,hapa tena niliamua kutoka kabisa nje ya mkoa wa mtwara,hili gari lilikuwa linaelekea dar es salaam,sehemu ambayo naenda lakini sijawahi kufika hata siku moja,sehemu ambayo sinauhakika kama nina ndugu,sehemu ambayo naisikia kwenye midomo ya watu na kuiona kwenye mikanda ya Tv tuu.

nilijisemea mwenye,mungu niongoze vyema juu ya hii safari ninayoianza kwamaana naamini wewe waijua vizuri mwanzo na mwisho wake.

**************ITAENDELEA************”👄👄👄

DOWNLOAD APPLICATION YETU SASA KWA MUENDELEZO NA SIMULIZI NZURI ZA KUSISIMUA OFFLINE.
👉https://play.google.com/store/apps/details?id=com.godstarapp
SAMBAZA KWA WENGINE NA HUKO MBELE NDIO KUTAMU ZAIDI
TAZAMA MWANZO WA SIMULIZI HIZI HAPA 👉 MWANZONI

No comments:

Post a Comment