Breaking

Friday, September 4, 2020

UTAMU WA MAMA Sehemu ya 63

 

UTAMU WA MAMA SEHEMU YA 63
MTUNZI: GODFREY GODSTAR
CONTACT: 0717069756
FB PAGE: https://www.facebook.com/godstaronline/
AGE:18+
SEHEMU YA 63

#ENDELEA_NAYO

gari ilianza safari huku kigiza bado kikiwepo na kamwanga kwa mbali kikawa kinaonekana,nililikumbatia vizuri begi langu la nguo kutokana na baridi kali ingawa nilikuwa nimevaa sweta nilolokabidhiwa na madame vero,nilihakiki pesa zangu na kujiridhisha kuwa ziko mahali salama kabisa.
masumbuko mie nikawa nimezama mazima kwenye ulimwengu wa mawazo,kila nilipotafakari nilijiona kuwa ni mpumbavu mkubwa,nikajisemea mwenyewe mapenzi yameniponza mie leo nakimbia mji ambao ndio umenilea na kunisomesha,nakuwa mkimbizi wa kwenda katika miji ya watu dah,masumbuko mie ni pepo gani sijui limenikumba.

pasipokujitambua usingizi ulinishika hapohapo kutokana na usiku sikupata usingizi kabisa,ila kabla sijapata kusinzia vizuri alikuja kondakta anayekatisha tiketi na mimi nikatoa pesa na kunipatia tiketi,baada ya tukio hilo kupita sikukumbuka tena kilichoendelea ndani ya gari ila nilikuja kustuka kutoka kwenye usingizi mkali baada ya gari kusimama na kwenye madilisha ya gari kukipita wafanya biashara,kuna aliyebeba vinywaji,kuna anayeuza mayai,kuna anayeuza maziwa n.k ilimradi kila mmoja atetee familia yake.
macho yangu yalipoangaza nje niligundua kuwa ni kituo cha basi ila kipengele ilikuwa ni kujua ni kituo gani kile cha basi na tupo wapi,ikanibidi nimuulize jilani yangu na yeye akaniambia kuwa hapa ndio lindi mjini.
duh nilistaajabu sana na pia nilifurahi maana huu mkoa nilikuwa nausikia tu midomoni mwa watu ila leo nimeuona laivu bila chenga.

hapa hatukuchukua muda mrefu safari ikaanza tena,hakika ilikuwa ni safari ndefu sana.

mida ya saa 4 gari yetu iliingia kwenye sehemu ya kupata chakula na hapa nilikuta magari mengine yanayoenda dar na yanayoenda Lindi na mtwara,niliposhuka kwenye gari nilistaajabu kuona wanawake kibao wakiwa wanafanya biashara ya kuuza samaki,hakika kuna samaki wengi sana tena sana,kila aina ya samaki wa kukaanga walikuwa hapo,wakati najiuliza hapa ni wapi,gafra nilijibiwa na kipaza sauti kutoka kwa mshehereshaji wa eneo hili.
"karibuni ndugu abiria,poleni kwa uchovu wa safari,hapa ndipo nangulukuru,unaweza kupata chakula kile ukipendacho"

haa nikabaki na butwaa na kujisemea kumbe hapa ndio nangulukuru sehemu ambayo kunasifika kwa samaki wengi,daah hapa masumbuko wala sikuhitaji tena kuhadithiwa ila mboni za macho yangu zilitosha kunihakikishia na kuniaminisha kuwa hapa kuna samaki wengi,mwanaume sikutaka kupoteza muda na moja kwa moja nilielekea kwenye banda moja la samaki na kununua samaki ninaowataka na nikachukua na soda yangu moja pamoja na maji kisha nikarudi ndani ya gari.

wakati naanza kula simu yangu ambayo nilikabidhiwa na madame vero ikawa inaita na nilipoangalia kwenye kioo ilikuwa ni namba tupu haikuwa na jina,niliipokea na moyo wangu ulifanya paa baada ya kuisikia sauti ya madame vero.

"niambie kipenzi,umefikia wapi muda huu?"

kwa tabasamu huku nikila nikamwambia nipo nangulukuru madame.

"ooh sawa,sasa yule mtu niliyekuambia atakuja kukupokea utamkuta palepale nilipokuambia ushukie sawa na namba nakutumia ili uwasiliane naye sawa"

nikamwambia sawa na hapohapo akakata simu.

nakumbuka kabla ya kuondoka madame aliniambia "kuna mdogo wangu wa kiume nilishamuelezea kuhusu ujio wako atakupokea na utakuwa unakaa kwake sawa"

Hakika safari ya kufika dar es salaam ilikuwa ni ngumu sana,maana nilikaa kwenye kiti hadi nikahisi endepo nikinyanyuka hapa ngozi naweza kuiacha kwenye siti ya gari.

upweke husiokuwa na mtu wa kupiga naye stori ndio ulinifanya nilale kila mara,niliupiga usingizi wa kwenda kwa muda huu.

nikaja kustuka tena na kuona bado safari inaendelea,saa 10 jioni gari liliingia dar es salaam na kufika kituo kimoja cha basi cha mbagala rangi tatu,sikuwa nakifahamu kinaitwaje ila nilipata majibu baada ya kuuliza hapa panaitwaje,miongoni mwa abiria ambao walikuwa wanashuka hapo na mimi nilikuwa ni mmoja wao.

nilivaa begi langu mgongoni na kushuka chini,nikawa naangalia msongamano wa watu.
niliitoa simu yangu na kumpigia mwenyeji wangu ambae niliambiwa anakuja kunifuata,kweli wakati napiga na kupokelewa,kumbe niliyekuwa nampigia alikuwa yupo pembeni yangu,nilikata simu baada ya kugundua ninayeongea naye nipo naye.

tulisalimiana na tukaanza safari ya kuelekea kwake.

**************ITAENDELEA************”👄👄👄

DOWNLOAD APPLICATION YETU SASA KWA MUENDELEZO NA SIMULIZI NZURI ZA KUSISIMUA OFFLINE.
👉https://play.google.com/store/apps/details?id=com.godstarapp
SAMBAZA KWA WENGINE NA HUKO MBELE NDIO KUTAMU ZAIDI
TAZAMA MWANZO WA SIMULIZI HIZI HAPA 👉 MWANZONI

No comments:

Post a Comment