Breaking

Friday, September 4, 2020

UTAMU WA MAMA Sehemu ya 64


 UTAMU WA MAMA SEHEMU YA 64

MTUNZI: GODFREY GODSTAR
CONTACT: 0717069756
FB PAGE: https://www.facebook.com/godstaronline/
AGE:18+
SEHEMU YA 64

#ILIPOISHIA

tulisalimiana na tukaanza safari ya kuelekea kwake.

#ENDELEA_NAYO

tulifika kwenye kituo cha mabasi na lilikuja gari lililoandikwa mbagala makumbusho,tukalipanda hilohilo.
hakika macho yangu hayakutulia kabisa,yalikuwa yakiangaza kila pande,niliyaona mengi hasa wanawake wa dar es salaam walivyokuwa warembo,niliwaona wanawake wa aina mbalimbali,wenye maumbo mbalimbali na rangi mbalimbali ni tofauti na kijiji nilichotoka mimi maana kumkuta msichana mweupe kama muarabu ni nadra sana ila kwa dar ni mashallah.

nilibahatika kuliona bango kubwa lililokuwa linasomeka dar live,nikawa najiuliza hapa ndio dar live ile ambayo niliyokuwa naisikia kwenye radio newala au ni jina tu mtu amelipenda,nilitafakari mwisho nikaona ujinga kwanini nisiulize wakati mwenyeji wangu yupo,nilipomuuliza mwenyeji wangu akaniambia ile ndio dar live ambayo wasanii mbalimbali huwa wanatumbuiza hapo.

jamani dar ni nzuri na yenye kupendeza,nilikuwa nikiangalia kama nitabahatika kuiona nyumba ya udongo lakini wapi,sikupata bahati hiyo kabisa,nilimsikia konda akisema "taifa" na abiria mmoja akajibu "shusha" nilipotazama nje ya gari niliuona uwanja mkubwa wa mpira,hapa sikutaka kuuliza wala kujuzwa ila jibu lilikuja moja kwa moja kuwa huu ndio uwanja wa taifa,hakika nilijikuta natabasamu na mwisho nikasema kwakuwa nipo dar lazima siku moja niingie mule.

safari ilitupeleka hadi kwenye kituo kimoja kinaitwa magomeni mikumi na hapo mwenyeji wangu akaniambia tumefika tushuke.

kitendo cha kushuka tu macho yangu yaligongana na bint mmoja mzuri na bila shaka alikuwa ni mtoto wa kiarabu hakika sikusita kumtazama kwa jinsi alivyokuwa mzuri ingawa yeye hakuwa na habari na mimi hata kidogo.

mwenyeji wangu alinikatisha mitaa hakika kila tulipopita nilikuwa nakisikia kiswahili tu kikiongelewa ni tofauti na nilipotoka maana kumetawaliwa na lugha ya kimakonde tupu,yaani ukiona watu wanaongea kiswahili basi tambua ni mtu amekaa sana dar es salaam.

tulifika kwenye nyumba moja na bila shaka ilikuwa ni nyumba yenye wapangaji kwa jinsi nilivyoona.

"eeh frank bora nilivyokuona,ndio nini amenidanganya Jana?"

alikuwa ni dada mmoja ambae alilitaja jina la frank,ndipo na mimi nikajua kumbe huyu mwenyeji wangu anaitwa frank.

"aah na wewe ushaanza wewe hauoni nipo na mgeni unaanza kunitia aibu bwana"

yule dada alicheka baada ya kujibiwa na frank.

nilipopiga jicho pembeni nilimuona dada mwingine akitoka ndani,alikuwa ana rangi nyeusi ya mng'ao,hakika urefu wake ulimfanya azidi kuonekana ni mrembo zaidi,masumbuko mie nilijisemea tu ndani ya moyo "shetani unikome maana nilisikia kwamba mjini kila kitu cha mtu na kila mtu wa mtu.
tuliingia ndani na jamaa akanikaribisha na kuniambia niketi.

"pole kwa uchovu wa safari mdogo wangu"

bila kusita nikamjibu ahsante ila gafra simu yake ikawa inaita aliipokea na kuanza kuongea ila kwa yale mazungumzo nilijua fika ni madame vero na mwisho frank akanikabidhi simu na kuniambia Dada anataka kuzungumza na we we na Mimi niliichukua simu.

"vipi kipenzi,umefika salama?"

madame alikuwa ni mtu wa furaha tu muda wrote kwangu ingawa nilimuona katili ile Siku aliyokuja kujua kwamba ninatembea na mdogo wake na nimeshampa mimba.

"masumbuko naomba unisikilize kwa makini,Mimi nakupenda na tambua huku umemuacha angel akiwa na mimba,tafadhali nataka hapo utoke,nitakutumia pesa ya pango na pesa ya kufanya vijibiashara vidogovidogo ili maisha kwa upande wako yaendelee"

hakika madame wakati ananiambia haya,machozi yalikuwa yananilenga,maana nilikuwa najiuliza kwanini madame bado ananijali na ananipenda,mbali na ubaya niliomuonyesha,nikazidi kujiona wanini mimi,laiti ningetulia na madame vero leo nisingepata tabu kabisa,kweli mwana kulitaka ndio mwanakulipata.

nilimjibu madame kuwa nimekuelewa na nitafanya ulivyoniambia.

"pole ndugu yangu kwa matatizo yaliyokukuta,sisi vijana hivyo changamoto kama hizo zipo,karibu dar na hapa ni nyumbani kwako,mimi naitwa frank,ni ndugu baba mkubwa na mdogo na veronika,yaani yule ni dada yangu,yeye ni mkubwa kwangu"

dah frank alikuwa anaongea na nilivyokuwa namtazama alikuwa ni mtu mcheshi na sio wa majivuno.

"wewe frank,frank ebu njoo kwanza"

ilikuwa ni Sauti ya mtoto wa kike ikimuita frank ila kabla frank hajaitikia wala kutoka yule msichana aliingia yeye,mtumee bint alikuja akawa amesimama mlangoni,sasa ule mwanga wa nje uliokuwa ukipiga pale mlangoni wate alikuwa ameuziba yeye,alikuwa amevaa dera tu na ule mwanga ulidhihirisha fika kuwa ndani hata chupi hakuvaa kabisa.
mmh niliguna na kujikuta nainamia chini kwa aibu,yaani Mimi ndio nikawa naona aibu na nilipomwangalia miguuni nilimuona amevaa shanga tena miguu yote miwili,nikapatwa na hofu maana kwetu Kyle ukimuona MTU anavaa ushanga miguuni au shingoni na mikononi basi tabibu wa kienyeji au ana majini.

nilijikuta namuhurumia yaani msichana mzuri alafu ana majini.

"sikia frank hivi Leo zamu ya nani umeme"

"leo nafikiri ni mama amina,kwani ayupo au"

"ametoka nafikiri,ooh naona uko na mgeni mdogo wako au rafiki yako?"

"eeeh wewe tena farida ushaanza,mdogo wangu huyu sawa"

"hahaha frank bwana,si nauliza alafu mzuri,mambo best?"

dah huyu msichana alikuwa chenga balaa,alinipa mambo na Mimi nikamjibu powa,alipomaliza maongezi akatoka nje,huku nyuma aliacha balaa,yaani alikuwa mwembamba hana makalio makubwa ila yalikuwa laini na yanatikisika balaa,alipokwisha kutoka nikaona bora nimuulize frank "samahani kaka,huyu mbona amevaa ushanga miguuni ni mganga au anaumwa majini?

"hahahaha,wapi ni fasheni watoto wa mjini hao na urembo wao,ila yaumu ndani mdogo wangu yatazame tu na uwe mvumilivu,humu ndani walioolewa ni wawili tu ila wanawake waliobakia wote wadangaji"

nilimuelewa vizuri ila kwenye neno udangaji hapo ndio nilishindwa kumuelewa anamaanisha nini.
tulisalimiana na tukaanza safari ya kuelekea kwake.

**************ITAENDELEA************”👄👄👄

DOWNLOAD APPLICATION YETU SASA KWA MUENDELEZO NA SIMULIZI NZURI ZA KUSISIMUA OFFLINE.
👉https://play.google.com/store/apps/details?id=com.godstarapp
SAMBAZA KWA WENGINE NA HUKO MBELE NDIO KUTAMU ZAIDI
TAZAMA MWANZO WA SIMULIZI HIZI HAPA 👉 MWANZONI

No comments:

Post a Comment